Posts

RAIS WA UTPC AFURAHISHWA NA UBUNIFU WALIOONESHA WAANDISHI WA HABARI

Image
 Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania(UTPC)  Deogratius Nsokolo akiwa ameambatana na Wajumbe wa bodi ya UTPC wametembelea mabanda ya maonesho ya kazi wanazofanya wanachama  wa Umoja huo na kujionea namna ambavyo Waandishi wanafanya kazi za kihabari na kuibua changamoto kwenye jamii. Nsokolo amefurahishwa na namna ambavyo Waandishi wamekuwa wabunifu katika maonesho hayo ambayo yamefanyika katika viwanja vya Ofisi ya UTPC jijini Dodoma. Aidha Nsokolo amesema kupitia maonesho hayo Waandishi wameweza kuonesha shughuli za kiuchumi wanazozifanya na kujikita katika Habari za uchunguzi. Kwa upande wa mwakilishi wa Shirika la Twaweza ambao wamejikita katika kufanya tafiti za Sauti za Waandishi wa Habari Bi.Jane Shussa amesema ili Vyombo vya  habari viweze kupiga hatua na kuweza kujitegemea ni Lazima wao waweze kubadilika na kuandika Habari zenye ukweli. Naye,Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Kenneth Simbaya amesema maonesho hayo yamekuwa na faida kubwa na kuahidi kuwa mwaka ujao kuy

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

Image
 Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Deogratius Nsokolo amesema ili kusaidia kupunguza hali ya uhasama dhidi ya Waandishi wa Habari UTPC inaendelea kutumia Klabu za Waandishi wa Habari mikoani kuhamasisha na kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa Uhuru wa  vyombo vya Habari na jukumu la Waandishi wa Habari katika jamii.  Nsokolo ameyasema hayo Leo Novemba 2,2023 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa siku ya Kimataifa ya kukomesha Uhalifu dhidi ya Waandishi wa Habari ulioandaliwa na UTPC na kufanyika kwa njia ya mtandao(Zoom). Amesema maadhimisho hayo kwa mwaka 2023 yanalenga Kuongeza uelewa kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo Waandishi katika kutekeleza majukumu Yao,lakin pia kuonya juu ya kukithiri kwa vitendo vya kikatili na ukandamizaji dhidi ya Waandishi wa Habari. Aidha akiongelea kujenga Mazingira salama kwa Waandishi wa Habari amewashukuru ubalozi wa Uswiss hapa Nchini Tanzania,kwa ufadhili wao katika mradi na Mkuu wa jeshi la polisi Nchini IGP Camilius Wam

WAZIRI MKUU ATIMIZA AHADI YAKE KWA REYO

Image
 Taasisi ya vijana inayojishughulisha na utunzaji wa Mazingira mkoani Rukwa(Rukwa Environmental Youth Organization-REYO)imekabidhiwa Pikipiki ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa mapema mwaka huu alipofanya ziara katika Mkoa wa Rukwa. Amikabidhi Pikipiki hiyo kwa niaba ya Waziri Mkuu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere ameishukuru ofisi ya Waziri Mkuu kwa kutimiza ahadi hiyo kwa Taasisi ya REYO. Ameipongeza Taasisi hiyo kwa kuendelea kutunza Mazingira na kuhamasisha wananchi kutunza Mazingira kwa kutokata miti na kuchoma moto hovyo misitu iliyopo. Akipokea Pikipiki hyo kwa niaba ya Taasisi ya REYO,Be.Issa Rubega amemshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa msaada huo ambao itasaidia kuendelea kampeni Ya utunzaji Mazingira kwa kuwa Pikipiki hiyo itasaidia kufika kwa urahisi na haraka katika maeneo yote.

ZIMAMOTO YATOA MAFUNZO KWA WATUMISHI RUKWA.

Image
 Jeshi la zimamoto Mkoani Rukwa limetoa mafunzo ya uokozi,kujikinga na kukabiliana na majanga ya moto kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa. Mafunzo hayo yaliandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na jeshi la zimamoto Mkoa wa Rukwa yakiwa na lengo la kuwapa watumishi wa umma ujuzi wa kuzuia,kuthibiti na kukabiliana vyema na majanga ya moto. Mafunzo hayo yalitofanyika oktoba 12,2023 yamehusisha utoaji wa Elimu juu ya hatua mbalimbali ya za kukabiliana na majanga ya moto,taratibu za uokoaji,na Matumizi sahihi ya vifaa vya kuzima moto na huduma ya kwanza. Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa,Bi .Sabina Msongela Kaimu Katibu Tawala utawala na usimamizi wa rasilimali watu Mkoa wa Rukwa amewashukuru watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushiriki mafunzo hayo.Amesema kuwa Mafunzo hayo yataongeza kujiamini kwa watumishi wa umma katika kuzuia na kuthibiti majanga ya moto. Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Rukwa limeipongeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa kuan

KIKUNDI CHA WAVUVI KATA YA SAMAZI CHAPATA MKOPO WA BOTI NA ZANA ZA UVUVI

Image
 Wizara ya Mifugo na uvuvi kupitia Benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania TDB imesaini Mkataba wa mkopo wa boti ya uvuvi na zana za uvuvi Kwa kikundi Cha uvuvi Cha Umoja kilichopo kata ya Samazi Wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa kama hatua yakuwawezesha wavuvi kujikwamua kiuchumi. Akiongea ofisini kwake wakati wa hafla fupi ya kusaini Mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kalambo Shafi Mpemba,amesema mkopo huo una thamani ya Shilingi Milioni thelathini na Saba na kwamba umetolewa kwa ajili ya ununuzi wa boti aina ya Fiber,nyavu,mashine na kifaa Cha kutafutia samaki ziwani. Licha ya Hilo Mpenda aliipongeza Serikali ya awamu ya sita kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mkopo huo pamoja na boti mbili zenye thamani ya milioni 108 ambazo kwa pamoja zinaenda kusaidia kudhibiti uvuvi haramu,Udhibiti na usimamizi wa rasilimali uvuvi katika kata ya Kasanga na Samazi katika mwambao wa Ziwa Tanganyika. Kwa upande wake diwani wa kata ya

WAGANGA WAKUU WA MIKOA WAAGIZWA KUKAMILISHA MAANDALIZI YA CHANJO YA POLIO

Image
 Waganga wakuu wa Mikoa ya Rukwa ,Songwe,Katavi,Mbeya na Kagera wametakiwa kukamilisha maandalizi ya Kampeni ya kitaifa ya chanjo dhidi ya Polio inayotarajiwa kufanyika tarehe 21 hadi 24 Septemba 2023. Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Tumain Nagu ametoa maelekezo hayo Leo tarehe 15 Septemba 2023 alipofanya kikao na watumishi wa sekta ya Afya mkoani Rukwa. Profesa Nagu ametoa maelekezo kwa waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya zilizomo katika mikoa hiyo kukamilisha maandalizi kabla ya tarehe hizo. Amesema kuwa polio ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababisha ulemavu wa viungo na unaoweza kusababisha kifo.Njia mojawapo ya maambukizi ni kupitia kinyesi hivyo ametaka wananchi wote wakumbushwe na kuelekezwa kuwa na vyoo Bora na kuvitumia kwa usahihi. Amewataka waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha watoto wenye umri wa miaka nane kushuka chini anafikiwa pasipo kujali changamoto za kijiografia . Amewaeleza kuhakikisha chanjo inapatikana katika maeneo yote yaliyotengwa kwa shughuli hiyo na kuhakikis

RUKWA YAPONGEZWA MAANDALIZI YA UDTHIBITI POLIO

Image
 Mganga Mkuu wa Serikali Pro.Tumain Nagu ameipongeza timu ya uendeshaji wa Huduma za Afya ngazi ya Mkoa (RHMT) ya Mkoa wa Rukwa kwa maandalizi na hatua za haraka zilizochukuliwa baada ya kisa kimoja Cha Polio kuripotiwa hapo tarehe 26 Mei ,2023. Ameyazungumza hayo Leo Septemba  14,2023 alipofanya kikao na timu ya uendeshaji wa Huduma za Afya ngazi ya Mkoa (RHMT) wakati wa kujadili na kukagua maandalizi ya Mkoa wa Rukwa kutoa chanjo dhidi ya polio  Mganga Mkuu wa Serikali atafanya ziara katika Halmashauri ya Manispaa Sumbawanga ambapo atatembelea kituo Cha Afya Mazwi na Zahanati ya kilimahewa,pia atatembelea Halmashauri ya Wilaya Nkasi ambapo atatembelea hospitali ya Wilaya ya Nkasi na kituo Cha Afya Nkomolo. Profesa Nagu,amesisitiza kuwa watoto 391,883 walilengwa wapatiwe chanjo ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Polio ugonjwa huo ambao unaathiri watoto chini ya umri wa miaka 05 hadi 15.